waja-schools

Baadhi ya Halmashauri zimeelezwa kutumia vibaya Fedha za Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli  amesema fedha za Halmashauri zinatakiwa kutumika ipasavyo kwa lengo la kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo na sio vinginevyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Wilayani Chato wakati wa makabidhiano wa Nyumba 50 za watumishi wa sekta ya afya pamoja na mtambo wa kuchujia mafuta ya alizeti.

Rais Dk Magufuli amesema fedha za Halmashauri zimefanywa ni za baadhi ya watu na kuzifuja huku Madiwani wakichukua miradi wenyewe na kuwa Wakandarasi.

Wakazi wa Chato wakifatilia Mkutano

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamine Mkapa akizungumza na Wananchi pamoja na Watendaji mbalimbali juu ya Taasisi ya Mkapa ambayo imejikita kuboresha sekta ya Afya. 

Rais Mstaafu Benjamine Mkapa akimkabidhi rasmi hati ya nyumba 50 za Watumishi wa Afya  kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amewahakikishia Wananchi kuwa sasa Serikali inanunua Dawa kwa wazalishaji na wategemee bei nzuri ambayo kila mwananchi ataimudu.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Joseph Msukuma amemuomba Rais Magufuli pindi fedha za makinikia zikilipwa auangalie Mkoa wa Geita kwa kuwapa fedha ili wazielekeze kwenye huduma za Elimu,Afya na kadhalika. 

Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akikabidhi hati ya mradi wa mtambo wa kuchuja Mafuta ya Alizeti.

Rais John Magufuli akiondoka katika Uwanjani baada ya kumaliza kuzungumza na Wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *