waja-schools

Baadhi ya Watu Wanadaiwa Kusambaza Taarifa Zisizo za Kweli Juu ya Kifo cha Mawazo

Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie amesema kuna dalili za baadhi ya watu kutaka kuchafua amani iliyopo Wilayani hapo kwa kutoa taarifa zisizo na ukweli juu ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Alphonce Mawazo huku na baadhi ya watu kutishiwa maisha.

Amesema kuwa zipo taarifa za kiintelijensia na pia ushahidi wa ujumbe mfupi unaotishia kuwaua viongozi wa vyama vya siasa Wilaya na Mkoa wa Geita wakihusishwa na tukio la Kifo cha Mawazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *