waja-schools

Benki ya CITI wakubali kushirikiana na Mkoa wa Geita katika utekekezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa CITI BANK Joseph Carasso Junior  ambapo wamekubaliana Bank hiyo kushirikiana na Mkoa wa Geita katika utekekezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati yenye lengo la kuinua kipato na kuleta maendeleo kwa Mkoa.

CITI Bank wameonesha nia katika uwekezaji wa miradi ya Kilimo na uwezeshaji wa vijana ambapo wameahidi kuukumbuka mkoa wa Geita kwa kuuweka katika program yao ya mwaka huu.

Wakati huo huo Mhe.Robert Gabriel amefanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya ujenzi ya Hyuna kutoka China ambao wemeonesha nia ya kuja Geita kuwekeza katika sekta ya Viwanda vya ngozi na kuunganisha piki piki wameahidi kufika Mkoani Geita mwezi juni 2018 kwa ajili ya kujionea mazingira lakini pia kufanya mazungumzo ya kina kuhusu uwekezaji huo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *