waja-schools

Bomu laua Watu wawili na kujeruhi mmoja

Tukio hili limetokea kijiji cha Mrahamba Kata ya Nkome Wilaya ya Geita

nadaiwa majira ya saa tisa june 30  mchana watoto walikuwa wanacheza maeneo ya shamba hili na wakaona kitu ambacho walihisi ni vyuma tu wakakibeba na kuondoka nacho ambapo walifika anapoishi William Jije(32) na kumuonyesha na alipolichukua lilifungua na mocha kutoka kisha kulipuka.

 

William alifariki pale pale na mtoto Denice Faida (4) alikimbizwa hospitali lakini bahati mbaya alifariki

Emmanuel Juma ambaye alikuwa na Marehemu Denice wakati wakiokota bomu lakini walipofika na kumpa William na kufungua Mtoto huyu alipoona moshi alikimbia na kunusurika kufa. 

Kamati ya Ulinzi na Usalama imefika hapa na kuwataka Wananchi kuwa makini wanapoona vitu vigeni waisiviguse bali watoe taarifa ili wataalamu waje kuchunguza. 

Mke wa Marehemu William,Regina Patrick ambaye amelazwa baada ya kupata majeraha kichwani na mkononi na hali yake inaendelea vizuri ambapo Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi amefika na kumjulia hali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *