waja-schools

Chuo Kikuu Huria Tawi la Geita lazindua Mwaka mpya wa Masomo

Wanachuo wapya na wa zamani wa Chuo kikuu huria tayari kuzindua mwaka mpya wa masomo.

Pamoja kuonekana Chuo Kikuu Huria Tawi la Geita kusaidia kuongeza wasomi ambapo kwa sasa wimbi kubwa la vijana wanajiunga na wengine wakiwa Watumishi lakini bado Wanachuo wanakabiliwa na ukosefu wa Majengo na vifaa vya kujifunzia hali inayowapa wakati mgumu wa kujifunza.

Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria Tawi la Geita Ally Abdu  amesema wameshapata jengo na kufanyiwa ukarabati kinachoendela ni kutafuta computer,usafiri lakini pia wamepata kiwanja ambacho muda si mrefu waatanza ujenzi.

 

 Rais wa Chuo hicho Faraja Manya wakati wa uzinduzi wa mwaka mpya wa Masomo amesema wamekuwa na wakati mgumu wa kukosa vifaa kama komputa na Majengo hasa ukiangalia wengi wanaosoma wanatoka maeneo ya Vijijini.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa masomo Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi amesema nafasi ya kusoma chuo huria ni fursa kwani unakuwa na uwezo wa kufanya kazi zako lakini pia gharama inakua nafuu.

Adelina Kabakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *