waja-schools

Hekari 270 ya Mashamba yadaiwa kuathirika na Sumu ya Zebaki

Ekari 270 za mashamba ya wakulima kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu iliyotoka kwenye Bwawa la kuhifadhia Kemikali lililopasuka kingo zake na maji kusambaa kwenye mashamba hayo.

 

Bwawa la kuhifadhia maji ya kemikali ambalo limeharibika na kusababisha maji mengi kuelekea kwenye shughuli za wananchi.

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola  akiangalia baadhi eneo ambalo limepasuka.

Ekari 270 za mashamba ya wakulima kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu iliyotoka kwenye Bwawa la kuhifadhia Kemikali lililopasuka kingo zake na maji kusambaa kwenye mashamba hayo.

Hali hiyo imemlazimu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bw Kangi Lugola kuitaka kampuni ya Madini ya Nyarugusu inayohusika na suala hilo kuwalipa fidia wananchi 57 ambao mazao yao yameathirika.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Kangi Lugola  akitembelea na kuangalia miche ya miti ambayo imekwisha kuathirika.

 

Moja kati ya wakurugenzi wa Mgodi wa  Nyarugusu Mine Co.Limited  Fred Masanja akionesha cheti NEMC ambacho naibu waziri alikikata.

Mkurugenzi wa Nyarugusu Mine Company Bw Fred Masanja amesema kusimamishwa kwa shughuli zao kunaweza kuathiri ytendaji wao kwa kuwa Tani Laki moja na 20 hawataweza kuzizalisha na hivyo watapata hasara ya zaidi ya Sh Milioni 600 hadi 700

Awali Naibu Waziri  Lugola aliagiza muwekezaji huyo akamatwe kutokana na kile alichodai kuwa ni uvunjifu wa sheria za utunzaji wa mazingira mgodini hapo na kwamba uongozi wa mgodi huo ulimzuia Afisa Mazingira wa Wilaya ya Geita Bi Hellen Eustace kutekeleza majukumu yake baada ya kufika mgodini hapo kukagua namna wanavyozingatia utunzaji mazingira

Naibu Waziri Kangi amesema Mwekezaji haruhusiwi kuendelea na shughuli anazozifanya na kufunga mgodi huo hadi watakapotekeleza mambo waliyoelekezwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *