waja-schools

Kili Challenge mwaka 2018 inatarajia kukusanya dola za kimarekani laki tano zitakazosaidia mapambano dhidi Ukimwi

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) huendesha mnada kila mwaka wa kuchangisha fedha kutoka taasisi na mashirika mbalimbali na fedha zitakazopatikana zinasiaidia mapambano ya dhidi ya Ukimwi.

Kili Challenge ni mfuko unachangia juhudi za serikali  katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).

Kili Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 %  mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.

Wapanda mlima Kilimanjaro mwaka 2018 ambapo wataanza june 24 hadi june 30

Watoto wa Kituo cha Moyo wa Huruma wakitoa burudani katika hafla hiyo.

Vitu mbalimbali ambavyo vilinadiwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *