waja-schools

Kongamano la BAVICHA lafana Mkoani Geita huku Mjumbe wa Kamati kuu Fredrick Sumaye asema Uchumi wa Dunia ya leo unahitaji Viongozi wenye uelewa

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ambaye pia ni Mjumbe Kamati kuu na Mwenyekiti wa kanda ya pwani akiingia katika ukumbi wa Goldbelt Mjini Geita kwa ajili ya Kongamano la Bavicha mkoa wa Geita.

Sumaye ametoa neno katika kongamano hilo kwa kusema kuwa uchumi wa dunia ya leo unahitaji Viongozi mwenye uelewa na mtizamo mpana wa biashara kwani uchumi ni kielelezo muhimu kinachotoa taswira halisi ya nchi husika huku nchi zenye uchumi imara huwa na maendeleo mazuri na wananchi wake hufanya shughuli zao kwa kujiamini.

Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa geita Neema Chozaire akitoa risala na kusema 

Kongamano hili limewakusanya vijana kutoka Wilaya zote sita ambapo wameweza kubadilishana mawazo na mbinu mpya zitakazowasaidia katika maisha yao na jamii inayowazunguka.

Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita Neema Chozaire

Wanachama wakifatili Kongamano.

Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Viktoria Hasbet Ngurumoamewataka  Vijana ambao ndio mhimili mkubwa wa maendeleo kutumia muda  kujifunza maarifa yatakayowakwamua kiuchumi na hatimaye kulijenga taifa.

Mjumbe wa kamati kuu Fredrick Sumaye amewashukuru Vijana waliohudhuria Kongamano ambao wameonyesha ukomavu wa hali ya juu katika siasa na kuwataka kutorudi nyuma bali kusonga mbele kuhakikisha Chama kinasimama vizuri na kinakuwa na tija kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *