waja-schools

Kundi la Vijana liko katika hatari ya Maambukizi ya UKIMWI

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akipanda Mti kabla wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo Kimkoa imefanyika katika Kata ya Nyawilimilwa Kijiji cha Nyawilimilwa. 

Mkuu wa Wilaya Herman Kapufi akipanda Mti. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akipata taarifa ya hali ya upimaji wa UKIMWI. 

Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Japhet Simeo akisoma taarifa katika kilele cha Maadhimisho ya Ukimwi Duniani. 

Imeelezwa kuwa Ukimwi bado ni tishio kwa Mkoa wa Geita na tangu kampeni ya upimaji wa Virusi vya UKIMWI izinduliwe ambapo kila watu 100 wanaopimwa watu 3 hadi 5 wanakutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Taarifa ya utafiti wa hali ya UKIMWI uliofanyika mwaka 2012 ilionesha hali ni mbaya kwa kundi la Vijana,kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa Vijana wenye umri wa kubarehe ni kubwa hasa kuanzi umri wa miaka 15 hadi 25 na Wasichana wapo katika hatari zaidi ikilinganishwa na Wavulana.

Mkuu wa Mkoa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Watoto wenye uhitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akisoma baadhi ya mabango ambayo yanaonyesha kero za Wananchi ambapo ameahidi kuzitatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *