waja-schools

Mashindano ya Doto Cup kutoa vipaji vitakavyocheza timu za Taifa

Washiriki wa michezo mbalimbali wakiwa wamejipanga mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania Mohammed Kiganja. 

Michezo mbalimbali ikichezwa.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania Mohammed Kiganja ameona vipaji katika Michezo mbalimbali iliyochezwa na kutaka mwakani michezo hiyo ijikite kwa vijana chini ya miaka 18 na atatuma wataalamu kuja na kuangalia vipaji lengo ni kutoa fursa kwa vijana kupata nafasi ya kucheza timu za taifa.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko amesema ameanzisha Mashindano hayo ambayo kila mwaka yatakuwa yakifanyika yana lengo la kuibua vipaji vya vijana kupitia michezo. 

Agnes Japhet ambaye ni Mshiriki katika Mchezo wa mpira wa kikapu kwa Wanawake amesema changamoto ambayo wameiona ni ushiriki mdogo wa Wanawake kwani kuna baadhi hawaruhusiwi kushiriki michezo hasa walioolewa na kutaka elimu zaidi itolewe na watu waone umuhimu wa Michezo kwa Afya.

Ndimiyake Paul ameona michezo hiyo imewakutanisha kwa karibu na kubadilishana mawazo na kuomba kila mwaka yafanyike.

Anajulikana kwa Jina la Maria Rosa mtaalamu wa mbio za Baiskeli kilio chake ni kupatiwa vifaa kwani wamekuwa wakianguka na Baiskeli na kuumia kwa kukosa vifaa vya kujikinga. Washindi wa Michezo mbalimbali wakipatiwa zawadi zao ambapo kulikuwa na Zawadi za Fedha taslimu,Vyeti,Mbuzi na Kombe ambapo Timu ya Mpira wa Miguu ya Runzewe Academy iliibuka na Ushindi wa Doto Cup.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *