waja-schools

Mawaziri Wanne wa Uganda wavutiwa na Uwekezaji wa Madini Tanzania

Mawaziri wanne kutoka Wizara mbalimbali Nchini Uganda wamefanya Ziara Mkoani Geita kuangalia jinsi Gani Serikali ya Tanzania ilivyofanikiwa katika Sekta ya Madini aina ya Dhahabu na kubaini kuwa pamoja na kutembea baadhi ya Nchi za Afrika wameona Tanzania ni mfano wa kuigwa kwani wamefanikiwa kuwaendeleza wachimbaji Wadogo na kuwatafutia fursa mbalimbali.

Ni ziara ya siku moja ambapo Mawaziri hao wamepata nafasi ya kutembelea mgodi wa busolwa,Kadeo na mgodi wa mfano. 

Mawazili hao ni kutoka Wizara ya Madini,mambo ya Ndani,Waziri anayeshughulikia masuala mbalimabli Katika jiji la kampla pamoja na Uchumi.

Naibu Waziri wa Madini stanslaus Nyongo akizungumza na Waandishi wa Habari amesema  Serikali imewezesha fursa mbalimbali kwa Wachimbaji wadogo hali ambayo imewavutia pia mawaziri wa Uganda. 

 Lokeris Peter  ambaye ni Waziri wa nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda

 

Wadau wakitembelea Mgodi wa busolwa unaomilikiwa na Wanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema Mgodi wa Busolwa ni mfano wa kuigwa kwa kuweza kuwekeza kwenye sekta ya Madini na ni Mgodi mkubwa ambao umeweza kuzalisha ajira kwa Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *