waja-schools

Mvua yasababisha vifo vya Watoto Wawili

Watoto wawili wanaoishi katika Kijiji cha mwekako Kata ya Kasenga Wilayani Chato MkoaniGeita wamefariki Dunia kufuatia na mvua kubwa iliyonyesha Kijijini hapo.

watoto hao wa mzee Kurwa mmoja anakadiriwa kuwa na miaka 13 na mdogo miaka mawili.

Diwani wa kata ya Kasenga Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo madhara mengine yaliyojitokeza ni pamoja na uharibufu wa mali na miundombinu ya barabara.

Diwani wa kata ya Kasenga wilayani hapa Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema mbali na vifo pia mvua imesababisha uharibufu wa miundombinu ya barabara.

Aidha mvua hiyo imebomoa boma la zahanati lenye vyumba 17 ambalo bado lilikua linajengwa.

Uongozi wa kata unapita kwa wananchi kuangalia madhara yaliyojitoleza na kufanya tathmini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *