waja-schools

Ndege na magari yanayoingia Mgodi wa Dhahabu wa GGM kukaguliwa kwa lengo la kuziba mianya ya utoroshaji Madini

Serikali Wilaya ya Geita imeanza zoezi la kukagua kiasi cha madini kinachosafirishwa kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita ambapo kwa takwimu za mwezi juni dhahabu iliyokaguliwa ni kilo 1,867.771.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi akizungumza na Watendaji wa Kata za Mji wa Geita pamoja na Madiwani ambapo anaelezea juu ya umuhimu wa kukagua madini 

na amesema asilimia 0.3 ya uzalishaji waliyopaswa kulipwa sasa itakua halali kwakua watakau wamehakiki na kujiridhisha kwa dhahabu iliyotoka.

Kila jumatano GGM wanasafirisha dhahabu na serikali imeona wasimamie na kusaini kinachosafirishwa na wameteuliwa wajumbe watatu ambao ni afisa usalama ,mkuu wa polisi wilaya na Mkurugenzi wa mji.

Serikali ina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kila ndege inayotua na magari yanayoingia mgodini kukaguliwa ili kuziba mianya yote ya utoroshaji wa madini.

Pamoja na hayo 

Mkuu wa Wilaya ya Geita amefungua semina ya mafunzo elekezi kwa madiwani na watendaji wa kata wa halmashauri ya mji wa Geita ambapo imelenga kuwaelimisha namna ya kuibua miradi ya maendeleo kuanzia ngazi ya chini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *