waja-schools

Ng’ombe wavamia mashamba ya Wakulima

Zoezi la kuhamisha mifugo katika pori la akiba la Biharamulo lililopo mkoani Kagera ,sasa limekua kero kwa wananchi wa kijiji cha Mbuye kata ya Bwina wilayani Chato baada ya wafugaji waliokuwa katika maeneo hayo kudaiwa kuhamishia mifugo katika mashamba ya wakulima.

Wanachi wa  kijiji hicho wamedai ipo hatari ya kuibuka vita baina ya wakulima na wafugaji kufuatia makundi makubwa ya ng’ombe kuingizwa kwenye mashamba ya wakulima na kula mazao yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *