waja-schools

Nyavu za uvuvi haramu zenye thamani ya zaidi ya Milioni 100 zimeteketezwa

Halmashauri ya Wilaya ya Chato imefanikiwa kukamata nyavu haramu kuanzia januari hadi disemba mwaka 2017  ambapo jumla ya nyavu 7150 zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 huku watuhumiwa 21 walikamatwa kati yao kuna waliofungwa mwaka mmoja na miezi sita,wengine wamepigwa faini na kesi mbili bado zinaendelea Mahakamani.

Ni uteketezaji wa zana za uvuvi haramu walizokamata kuanzia oktoba hadi disemba 2017 zenye thamani ya zaidi ya milioni 100. 

Nyavu zilizokamatwa ni kokoro,Timba,nyavi ndogo za Makili,katuli,kadema,tupatupa,nyavu za dagaa na mitumbwi.

Mwenyekiti wa BMU Wilaya ya Chato Bashiri Manamba  amesema wamejitahidi kupambana na Uvuvi haramu lakini changamoto ni Wilaya jirani hazijajikita sana katika kukomesha na inaathiri kwa namna moja ama nyingine hasa kwa uwepo wa samaki wasiostahili kuvuliwa.

 Efasi MsenyaAfisa ni Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Chato amesema wamejipanga kuhakikisha doroa za mara kwa mara zinafanyika lakini pia wanashirikianai na kila kiongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha wanatokomeza suala la uvuvi haramu.

Kenned Bugigi ni Mvuvi anabainisha kuwa uvuvi haramu umewaathiri hasa kwa kukosa samaki kwa wingi kwani Wavuvi haramu wanavua hadi mazalia hali inayosababisha samaki kupungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *