waja-schools

Nyumba za Watumishi wa Sekta ya Afya zazinduliwa,Mkoa wa Geita,Simiyu na Kagera,zagharimu bilioni 2.5

Rais wa Awamu ya Tatu Benjamine Mkapa akizindua moja ya nyumba Wilayani Chato kati ya 20 zilizojengwa Mkoani Geita.

Moja ya nyumba iliyozinduliwa. 

Deogratius Rimoy n​i Afisa Mahusiano na Mawasiliano Taasisi ya Mkapa amesema lengo la miradi hii kuimarisha mifumo ya afya na sekta hii ilikumbwa ni uhaba wa watumishi maeneo ya Vijijini na hasa ukosefu wa maeneo mazuri ya kuishi karibu na kituo.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Mkungo Jasinta Kaijage amesema hapo awali walikuwa na changamoto kubwa ya nyumba ya watumishi na walikuwa wakiishi umbali wa kilomita mbili hali ambayo ilikuwa inawapa wakati mgumu mgonjwa wa dharura anapoletwa hapati huduma kwa wakati.

Mkazi wa Kijiji cha Mkungo akishukuru msaada wa nyumba ya watumishi na kusema kwa sasa huduma ni nzuri na wakija hata wakati wa usiku wana uhakika wa kumpata mganga na kupewa huduma kwa haraka.

Rais wa awamu ya Tatu Benjamine Mkapa akizungumza na Wakazi wa Mkungo Wilayani Chato baada ya kuzindua moja ya nyumba ya watumishi wa sekta ya Afya na kuwataka waone miradi hii ni yao na waitunze.

Rais wa awamu ya tatu Benjamine Mkapa akiwaaga Wakazi wa Mkunga baada ya kuhitimisha zoezi la uzinduzi.

Na july 10 

Nyumba hizo 50 za watumishi wa Afya mikoa ya Geita (20), Simiyu (20) na Kagera (10) zitakabidhiwa na Mhe. Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ataambatana na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja nao watakuwepo Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anna Mkapa, Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi , Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) Bi. Martha Abdul Setembo, na viongozi wa mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *