waja-schools

Ofisi za kuwawezesha wajasiriamali kimafunzo zitakazogharimu Milioni 520 kujengwa Chato na Geita

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji akiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk Charles Mwijage akiwa katika moja ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi zitakazogharimu Milioni 260 kwa kila Ofisi ambapo moja itejengwa Wilaya ya Chato na nyingine Geita Mjini.

Ofisi hizo zitakazotoa mafunzo ya Ujasiriamali na uchumi zikiwa Teknolojia za kisasa ambapo baada ya Mafunzo Wahitimu watakuwa na uwezo wa kuanzisha viwanda Vidogo wakiwa na sifa zinazohitajika na Mamlaka mbalimbali.

 

Mwenyeikiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola.

Akiwa Mjini Geita Waziri Dk Mwijage amepata nafasi ya kukutana na Wafanyabiashara ambapo baadhi yao wameomba ofisi muhimu kama TFDA na TBS ziwekwe karibu kwani kumekua na changamoto wanapotakiwa kutuma sampuli kwa ukaguzi zinakua zinapotea njiani na kutakiwa kutuma tena hali ambayo imedaiwa kuwa ni usumbufu.

Waziri Dk Mwijage akiwa katika Wilaya ya Chato amesema ifikapo mwezi wa nne Ofisi zikamilike na Chato kutajengwa mabanda kwa ajili ya shuguli za ujasiriamali.

 

Ofisi hizo zitakua na maabara ndogo kwa ajili ya uzalishaji,Chumba cha baridi kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa kama maziwa na kadhalika na kutakua na mabanda ya watakayotumia wajasiriamli kwa muda.

Wananchi waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya eneo litakalojengwa Ofisi na Mabanda.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk Charles Mwijage akizungumza pia na Mameneja wa Taasisi za Fedha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *