waja-schools

Usikose kuangalia kipindi maalum cha “Kili Challenge 2016”

Ni kumbukumbu nzuri ambayo utaingalia kupitia kituo cha Television cha ITV April 17 2017 saa nne usiku usikose.

Chini ni kumbukumbu za picha za Kili Challenge iliyofanyika mwaka 2016

Aliyekuwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter aliwapongeza wafanyakazi wote wa GGM,watu binafsi,mashirika ya kimataifa kama UNDP kwa kufanikisha kampeni hiyo ambayo mwaka huu imetimiza miaka 15

Mfanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Bw George Mandia (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Makamu wa Rais mwandamizi wa Anglo Gold Ashanti Mh Sicelo Mtuli (kushoto).Akishuhudia tukio hilo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Terry Mulpeter

Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) pamoja na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto na Banana Zoro wametoa burudani ya aina yake kwenye hafla ya kuwatunukia vyeti mashujaa waliopanda mlima Kilimanjaro kuchangisha fedha kusaidia waathirika wa janga la UKIMWI usiku wa Agosti 10 2016 kwenye ukumbi wa Desire Park mjini Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *