waja-schools

Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini awamu ya tatu yazinduliwa Mkoani Geita

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani akizindua mradi wa Umeme Vijijini awamu ya tatu katika Kijiji cha Nyijundu Wilaya ya Nyangh'hwale Mkoani Geita. 

Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu akibonyeza kitufe cha kuashiria uzinduzi umezinduliwa rasmi. 

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mjini ameishukuru Serikali kwa kuweza kusogeza huduma ya umeme vijijini na kuongeza kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 78.56 kwa ajili ya kugharamia kazi ya usambazaji umeme Mkoani Geita na Wananchi watumie fursa hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.

Naibu Waziri wa Nishati na madini Dk Medard Kalemani akiwapa baadhi Wazee kifaa cha umeme kinachoitwa UMETA(umeme tayari) kama zawadi kwao.

Mkurugenzi mtendaji wa REA Eng. Gissima Nyamo- Hanga amesema kiwango cha upatikanaji wa umeme bado ni changamoto na kuna vijiji 471 na vyenye umeme ni 85 tu sawa na asilimia 18 na mradi ukikamilika jumla ya Vijiji 305 vitakua na Umeme na kuongeza asilimia kufikia 64 hadi kufikia april 2019.

Mbunge wa jimbo la Nyangh'wale Hussein Kasu amepongeza mradi na kusisitiza kuna maeneo ya mradi kwa awamu ya pili nguzo zimeanguka Barabara ya kwenda Bukwimba na anaamini Mkandarasi mzuri atachaguliwa awamu hii na kutimiza lengo la mradi kwa faida ya Wananchi.

Eng. Amos Maganga ni Meneja Tanesco Kanda ya Ziwa amesema hivi sasa umeme unaotumika nchi nzima ni Megawati 1000 na mipango iliyopo ni kufikia mwaka 2020 kutakuwa na Megawati 3000.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani amesema lengo la Serikali ni kuona kila Mtanzania anakua na umeme na ndio maana Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 78.56 kwa Mkoa wa Geita kufanikisha umeme Vijijini. 

Mkandarasi kampuni ya White City ndio imepewa kazi ya usambazaji na kutakiwa kufanya kazi kwa uadilifu ili kuepusha malalamiko kutoka kwa Wananchi.

Wananchi wakifatilia uzinduzi wa REA

Afisa uhusiano wa Tanesco Mkoa wa Geita Emama Nyaki akimuelezea Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani juu ya kifaa cha UMETA.  Naibu Waziri wa Madini Dk Medard Kalemani akiwa katika picha na Viongozi na Watendaji mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *