waja-schools

Waandishi wa Habari wapewa mafunzo kuhusu miradi ya Mashirika ya UN Tanzania

Mafunzo hayo yamefanyika Mjini Kigoma yakiwa yamejumuisha Waandishi kutoka mkoa wa Geita,Kigoma,Tabora,Simiyu na Katavi.

Waandishi mbalimbali wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na UN Tanzania

Afisa Habari Mkuu Mashirika ya kimataifa(UN) Hoyce Temu akielezea ju ya malengo ya maendeleo endelevu ambayo yapo 17 .

Baadhi ya Malengo hayo ni la kwanza kufuta umasikini wenye sura zote kila mahali,la pili Kuondoa njaa,kuwa na usalama wachakula,kuboresha hali ya lishe na kukuza kilimo endelevu,la tatu kuhakikisha maisha yenye siha njema na kuboresha ustawi wa rika zote,la nne kuhakikisha elimu bora inayotolewa kwa usawa na kutengeneza fursa za kujiendeleza kwa wote.

Mwandishi wa habari leo Diana Deus

Mafunzo hayo ya siku moja yamelenga kuwajengea uwezo Waandishi ili waweze kuandika miradi kwa undani inayofanywa na Umoja wa mataifa Tanzania.

 

Mratibu wa Mpango wa pamoja wa (UN ) one Tanzania Evance Sangicha akiwasilisha mada juu ya programu ya pamoja ya kigoma ikiwa  inahusisha sekta mbalimbali mtambuka ya kieneo ya umoja wa mataifa unaolenga kuimarisha maendeleo na usalama wa watu wa Kigoma.

 

Mwandishi wa Habari Winnie Ngassa kutoka Uvinza Fm iliyoko Mkoani Kigoma akitoa mchango wake juu ya mada zilizowasilishwa.

Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima Salehe Mohammed.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *