waja-schools

Wamiliki wa Viwanda vya Kusindika bado hawana utaalamu bora wa Usindikaji

 

Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imewakutanisha wajasiriamali wanaosindika chakula mkoani Geita na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kutengeneza vyakula vinavyokidhi viwango vya usalama na vitakavyoweza kukuza soko la ndani na nje.

 

Kaimu Mkurugenzi usalama  wa chakula makao makuu ya TFDA  Bw Lazaro Mwambole akielezea dhumuni na malengo ya mafunzo hayo wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi.

Tafiti ambazo zilifanyika mwaka 2016 zilionekana kuwa wamiliki wengi wa viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazozitengeneza hali ambayo imesababisha kutokufanya kwa ubora zaidi usindikaji wao

Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita Bw Emily Kasaga amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha wanarutubisha vyakula ili view  salama na vyenye ubora kwa kuwa afya ya watumiaji iko mikononi mwao.

Baadhi ya washiriki  mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasimi na watumishi wa SIDO na TFDA.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *