waja-schools

Wananchi wafunga Barabara kwa ndoo za Maji lengo Mbunge aone kilio chao

Wakazi wa Kata na Kijiji cha Igulwa Wilayani Bukombe waamua kufunga Barabara kwa kutumia ndoo za maji kwa lengo la kumzuai Mbunge kupita ili aone na kuwasikiliza kero zao za Maji.

Wakazi wa eneo hili hasa wakinamama inawalazimu kuamka asubui na hata wakati mwingine usiku kwenda kutafuta maji na wakati mwingine wasiyapate. 

Visima vitatu ndio vinapatikana katika Kata hii na baadhi yake vimekauka kabisa 

Maji yanayopatikana katika Visima 

Dumu moja la Maji linauzwa kati ya 400 hadi 500 na wananchi hawamudu kununua.

Diwani wa Kata ya Igulwa Richard Mabenga akiwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko katika mkutano na Wananchi. Mheshimiwa Mbunge Doto Biteko amewaambia wananchi kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa Maji na mwaka huu wamepata fedha zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya kuwapatia maji wananchi wa Bukombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *