waja-schools

Wananchi walalamika kuchomewa nyumba,kuharibiwa mashamba na watendaji wa hifadhi.

Wakazi waliovamia Pori la Biharamulo Wilayani Chato wamesema pamoja na kuwepo kwa sheria inayokataza wananchi kuvamia hifadhi na kuanza shughuli za kibinadamu kama kilimo,ukataji uchomaji mkaa na ufugaji lakini hawakutendewa haki na Serikali kwa madai ya kufukuzwa katika pori hilo kwa kupigwa,kuchomewa nyumba zao na mazao kuharibiwa.

Wamedai kuwa laiti wangepewa muda wavune mazao yao na kuondoka kwa amani kuliko sasa ambapo zaidi ya kaya elfu moja hazina makazi tena ambapo kwa sasa kila familia imejihifadhi katika vichaka vilivyopo katika vjiji jirani wakiwa hawajui mustakabali wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *