waja-schools

Wanawake wa Kikundi cha Upendo wamaliza mwaka kwa aina yake

Kikundi cha Upendo kilichopo Mjini Geita kimefunga Mwaka kwa kugawana zawadi za upendo.

Kikundi hiki ni cha Wanawake Wajasiriamali na kinajihusisha na mchezo wa kukopa.

Ghati Joseph akimkabidhi zawadi ya Hotpots Scholastica mbogo

Scholastica Mbogo akifurahia zawadi alizopewa na Mwanachama Mwenzake. 

Blandina Boniphace akifurahi baada ya kupatiwazawadi ya mifuko ya saruji na Scholastica Mbogo.

Salma Mrisho akionyesha zawadi alizopewa na Blandina Joseph 

Salma mrisho akimkabidhi Catherine Msaki vyombo. 

Catherine Msaki akitoa zawadi ya upendo ya Simu kwa Lilian Ferdinand.

Lilian Ferdinand akionyesha Simu aliyonunuliwa. 

Catherine Msaki akisoma risiti inayoonyesha gharama ya Simu aliyomnunulia Lilian.  Leonia Kapalata amekabidhiwa risiti ya mifuko 10 ya Saruji na Lilian Ferdinand huku akifurahi na kuwaahidi Wanachama kuanza ujenzi wa Nyumba yake mara moja.

Leonia Kapalata akimpa zawadi Lilian Ferdinand

Leonia kapalala akimkabidhi zawadi za Nguo Ghati Joseph kwa niaba ya  Sara Dairusi ambaye atakabidhiwa zawadi zake.

Ester Kaijunga akiwa na furaha ya kukabidhiwa mifuko 12 ya simenti na Ghati Joseph.

 

Christina Felix akisubiri kwa hamu kupokea zawadi zake.

Hatimaye Christina Felix akipokea Mashuka kutoka kwa Ester Kaijunga.

Ghati Joseph akimuongezea zawadi ya Keki Catherine Msaki na kusisitiza ni upendo aliyonayo kwa Catherine.

 

Catherine akiwa katika pozi baada ya kupatiwa zawadi ya ndoo za rangi za silk mbili,nguo na viatu kutoka kwa Ghati Joseph.

Aina ya upeanaji wa Zawadi ni kuandika majina ya Wanachama ambapo kila Mwanachama ataokota kikaratasi na kukifungua jina atakalolipata ni siri yake hadi siku ya fungua tuone ndipo anamtaja liyemuokota na kumpa suprise.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *