waja-schools

Watakaochakachua fedha za miradi ya Afya na Elimu Mkoani Geita kukiona

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabrile amesema Miradi mingi imekua ikitumia fedha nyingi na mingine hata ikikamilika inakua bado haina tija kwa jamii na kutoa tahadhari juu ya fedha zilizotolewa na Serikali Shilingi milioni 400 katika Kituo cha Afya cha Kharumwa  Wilayani Nyangh’wale kuwa zisipotumika inavyotakiwa atahakikisha waliohusika kutafuna fedha wanachukuliwa hatua ili iwe mfano kwa watendaji na watumishi wa Umma.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Busolwa Wilayani Nynagh'wale wakiwa katika mstari kumsikiliza Mkuu wa Mkoa waliyetembelea katika Shule hiyo

Mkuu wa Mkoa ametaka Shule zilizopata fedha kujenga madarasa kwa kutumia mafundi wa kawaida ambao gharama zao hua nafuu lakini pia kuwawezesha kujiongezea kipato.

Mkuu wa Wilaya ya Nyangh'wale Hamimu Gwiyama.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameataka wanafunzi kusoma kwa bidii iliwafikie ndoto zao na kuwahakikishia kuwa Serikali inafanya kila namna kuhakikisha miundombinu inakua bora.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akishiriki ujenzi wa Shule ya Msingi Busolwa.

Rc Gabriel ametaka kila mradi unavyotekelezwa aletewe taarifa yote na kuona thamani ya mradi inaendana na fedha inayotumika au laa.

Ujenzi ukiendelea katika Shule ya Sekondari Nyijundu

Mwananchi aliyejitolea kuchangia ujenzi wa Zahanati kwa kuchangia fedha katika kijiji cha Bukulu Wilayani Nyang'wale

Zahanati ya Kijji cha Mwamakiligi Wilayani Nyang'hwale ambayo imezinduliwa rasmi kuanza shughuli ya kutoahuduma za afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *